SIJAWAHI KUPIGA PICHA ZA UTUPU NA WALA SIFAHAMIANI NA SINTAH : ASEMA RAYUU
Posted in Rayuu
Leo, Bongomovies.com Wamefanya interview kwa njia ya simu na mwanadada Rayuu alaice Bungenzi leo kuhusiana na mambo mablimbali yanayoandikwa kwenye mitandao na tovuti mbalimbali nchini. Katika interview hiyo tuliweza kupata mambo manne ambayo wapenzi wa filamu za kibongo hawayafahamu au wanaweza kuwa wameyasikia kinyume na ukweli kuhusu mwanadada huyu.
1. Hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza ili kupata umaarufu
Akiongea kwa msisitizo Rayuu amesema kuwa hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza kwenye mtandao kwa ajili ya kupata umaarufu.
“Sijawai kusambaza picha za utupu ili nipate umaarufu, hizo picha kweli ni zangu na ukizitazama vizuri sio picha za utupu kama watu wanavyosema, ni picha nilizopiga kwenye simu yangu kujiangalia tattoo yangu niliyochora kiunoni lakini kuna marafiki zangu waliochukua simu yangu na sijui ni nani ndio zilisambaa kutokea hapo na kila mtu kuandika stori anayoijua yeye” Alisema.
2. Hafahamiani na wala hajawai kuonana na sintah kwa zaidi ya miaka mingi sana
Rayuu amesema kuwa hajawai kuonana na sintah, wala hafahamiani naye personally na huwa anashangaa sana kwanini mwanadada huyu anamchafua kwenye blog yake.
“Kiukweli mi sifahamiani na Sintah, na wala hatujawahi kuonana kwa kipindi kirefu sana, sasa huwa nashangaa kwanini ananichafua na kunitukana kwenye blog yake. Kuna kipindi nilichoka nikaanza kumjibu lakini baadaye nikaona ni utoto bora ninyamaze kwanza nione kama ataacha lakini nashangaa hakui.
huyu dada mi huwa simuelewi kwakweli,anagombana na kila mtu, nahisi anaweza kugombana hata na panya. Kwanza ni mtu mzima sana kwangu. Nakumbuka mi namfahamu yeye wakati teyari kashakuwa maarufu na skendo za Juma nature na mimi nilikuwa bado mdogo sana. Sa sijui kwanini hakui. Kila siku anatukanwa kwenye blog yake lakini wala hajali.”…Alisema Rayuu
3. Marehemu Mzee Kipara ndiye haswa aliyemuingiza kwenye sanaa
Watu wengi hawajui kuwa marehemu mzee kipara ndiye aliyemuingiza Rayuu kwenye sanaa. Rayuu alisema kuwa anakumbuka siku moja kundi la kaole walienda kurekodi igizo lao mitaa ya nyumbani kwa kina Rayuu na alipowaona alimfuata mzee kipara na kumueleza nia yake na ndipo alipompeleka na kumtambulisha kwenye kundi la kaole na kuanza kupata nafasi ya kuigiza na kufanya mazoezi kundini hapo.
4. Sio mtu wa kutoka sana na akila "bata" anaumwa sana kesho yake
Rayuu amesema yeye sio mtu wa kutoka na kupenda kwenda club kama wengi wanavyodhani bali hupenda sana kushinda ndani kwani akifanya hivyo kesho yake lazima aumwe siku nzima

0 Maoni/comments: