"RED BRIGADE YA CHADEMA NI KUNDI LA KIGAIDI"....MWIGULU NCHEMBA.
Posted in
CCM,
Mwigulu Nchemba,
Red Brigade
Watanzania wenzangu,
Ni dhahiri kumekuwa na mijadala kadha wa kadha kuhusu vyama vya siasa
kuwa na vijana wao wa kuwa linda.
Nilionesha tofauti baina ya red
brigade na greenguard. Wanaojitetea wakakimbilia Dictionary bila kutumia
muda kufuatilia historia na chimbuko la kikundi hicho ambacho jina ,
matendo na malengo yake yako sawasawa na kule kilikoanzia.
Lakini
mjadala mkubwa ni kuhusu mpango wa CHADEMA kuanzisha jeshi lao la chama
chao, Jeshi ambalo halihitaji msaada wa polisi wala wa Jeshi la wananchi
wa Tanzania kwa mjibu wa kauli ya mkt wao mhe Mbowe.
Ni kinyume na
katiba ya nchi na hata katiba ya chama chao (pitia katiba yao).
Wanavunja katiba hiyo sio kwa bahati mbaya bali ni mpango wao unawabana
wa kuhakikisha amani ya nchi inatoweka .
Jeshi wanalotaka
kulianzisha si bahati mbaya,ni mpango wa siku nyingi hasa ukifuatilia
walikojifunzia ideology ya Red Brigade na aliyeileta CHADEMA.
MAANA HALISI YA RED BRIGADE NA WAANZILISHI WA HIYO TAASISI.
Red Brigade ilianzia ITALIA mwaka 1970 kwa kifupi ni BR,Wanzilishi
wake anafahamika kwa jina la Renato Curcio na Margherita(mara) Cagol
waliokutana wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Trento karibu na chuo
alichokuwa akisoma Dr Slaa.
Red Brigade ni kikundi kilichokuwa
kinajishughulisha na kuishambulia(kudhoofisha) serikali kwa kufanya
mambo mbalimbali ya Mauaji,Kuteka na Kuua wanasiasa, Kuhujumu kazi za
serikali, Kuiba mali za watu, Kupandikiza chuki kati ya wananchi na
serikali yao na wananchi na vyombo vya dola na Kufanya nchi isitawalike
(Rejea kauli ya Dr.slaa "NCHI HAITATAWALIKA"
Kikundi hiki kilikuwa
kinatumia mwamvuli wa kuwa na uchungu na mali za umma lakini badala yake
kikatumika , kuteka, kua na kumwagia sumu watu.
NOTE: Nazism
ya Ujerumani chini ya Hitler ilijipambanua kama Socialist party(lakini
matendo yake yalikuwa ni tofauti kabisa,Ugaidi na kuua ndio sifa yao).
Hiki kikundi kilivuma sana miaka ya 1970 hadi miaka ya 1980 (Hiki
kipindi Dr.Slaa alikuwa Italia kwenye masomo na maisha yake yalikuwa
huko). Red Brigade wakati huo walikuwa na kazi kubwa ya kuidhoofisha
serikali iliyopo madarakani chini ya waziri mkuu Aldo Moro wakati huo.
Mwaka 1978 kilianzishwa kikundi kikubwa zaidi ndani ya RED BRIGADE(Ndio
hicho chadema wanataka kukianzisha).Baada ya kuanzishwa kwa kikundi
hicho kikiwa na watu 1000,kikundi hiki kilifanikiwa kumteka waziri mkuu
Aldo Moro na kumuua Kinyama
Kuanzia mwaka 1974 hadi 1988
kikundi hiki kilifanya matukio ya kuteka, kuua,kumwagia sumu watu kwa
matukio zaidi ya 50.Na yote haya yalilenga kufanya serikali ya Italy
Isitawalike(DESTABALISE)..
KUKUA NA KUVUMA KWA RED BRIDGADE.
Matukio ya kuua na kuteka,kumwagia sumu na kuleta vurugu kila kona ya
Itali kiliwafanya Red Brigade kusikika sana nakuleta hofu kwa watu.
Walikuwa wanaua na kuteka kwa USIRI mkubwa tena wakiwa wanatembea chini
ya mwavuli wa chama cha kisiasa LOTTA CONTINUA na Potere Operaio.
Pia kilivuma sana kupitia Movement for Change MFC waliyoianzisha na
baadaye kuipa jina la MOVIMENTO SOCIALE ITALIANO(MSI) bila shaka ndio
M4C ya CHADEMA.
Ilikuwa ni miaka ya 1980 ambapo hiki kikundi
kilizimwa kabisa kabisa na serikali.Serikali iliamua kuchukua hatua
nzito kwa kuanzisha slogan ya ANTI-BR.
Yapo mengi sana ya kuelezea kuhusunia na kikundi hiki,(Pitia link hapa chini).
VIONGOZI WA RED BRIGADE WAKIMBIA ITALI.
Baada ya kusambaratisha Italia,RED BRIGADES wakakimbilia nchi
zingine,Mfano Antonio Negri na Cesare baltisti walikimbilia France.
Wengine walikimbilia Palestina.
Takwimu zinaonesha zaidi ya watu 780 waliuawa na kumwagiwa sumu Italia
chini ya BR,Lakini pia walifanya matukio zaidi ya 1400 ya uvunjifu wa
amani na kuifanya Italia isitawalike.
Tafiti zinaonesha Red
Brigade inaendelea kuishi kwenye nchi mbalimbali kupitia vyama vya
siasa,Na moja wapo ni India,Tanzania(CHADEMA) Amerika kusini n.k
Pitia Link hii>>https://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades na hiihttps://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades.
ALIYEILETEA CHADEMA KIKUNDI CHA RED BRIGADE NA MABADIRIKO YA BENDERA YA CHAMA.
Wakati wote haya ya RED BRIGADE yakiendela huko Italia,Kulikuwa na
Mtanzania mwenzetu akiishi na kusoma huko (mambo ya kanisa),Ni katibu
mkuu wa sasa wa CHADEMA Dr.slaa, Huyu ndiye aliyeleta falsafa ya
kuanzishwa kwa kikundi hicho cha kihalifu chini ya mwavuli wa chama.
Historia inatuambia Mwaka 1977 Dr Slaa alifanikiwa kupata upadirisho,
Aliamua kujiendeleza kimasomo kwa kujiunga katika chuo kikuu cha
Ponfical Urban Cha Roma cha huko Italia karibu na chuo walipokuwa
wakisoma waanzilishi wa Red Brigade kipindi hicho Italy .
Alipokuwa Italia masomoni ndipo alipojifunza mbinu hizi za RED BRIGADE na hatimaye kuzileta CHADEMA.
Baada ya Dr.slaa kujiunga CHADEMA akaongoza ubadilishaji wa bendera ya
chama (Bendera ya CHADEMA imebadilishwa na kuwekwa rangi nyekundu kama
mwagaji damu Italy na aliyeasisi mabadiriko haya ni Dr.slaa akichukua
sehemu ya bendera ya Red Bridgade wa Italy)na uundwaji wa katiba mpya ya
chama yenye Red Bridgade(jina hili alilitoa Dr.slaa kwa kuiga lile la
kikundi cha Italy) ndani.
Dr.slaa alipojiunga CHADEMA amekuwa mstari ma mbele kutengeneza mahusiano na Italia ya kisiasa
Kwa mara ya kwanza CHADEMA walipeleka vijana zaidi ya 50 kwenda
masomoni Italia kujifunza mambo ya Red Bridgade kwa mwavuli wa mafunzo
ya siasa na utawala.
RED BRIDGADE YA ITALIA(CHADEMA) NA KINACHOTOKEA NDANI YA NCHI YETU.
Ni wazi kabisa kabisa,Nchi yetu imekuwa ikikumbwa na mikasa ya uvunjifu
wa Amani, kutekwa kwa watanzania wenzetu,Kuuawa kwa wananchi, Kutekwa
na kuuawa kwa wanasiasa wenzetu kama ndago na mipango ya kuteka
wandishi.
Kubwa zaidi tumeshuhudiwa Kiongozi mkubwa wa chadema akisimama
jukwaani na kujinasibu "NCHI HAITATAWALIKA"(DESTABALISE). Na kuwambia
maaskofu wasiombee Amani
Ni ushuhuda ambao kila mtanzania anaweza
kuusema,Mikutano inayoua niyachadema,Wanaoteka na kumwagia tindikali
(sumu) ni vijana wa CHADEMA,Wanaojiita RED BRIDGADE ni CHADEMA,wanaoteka
watu hao hao wanahusishwa ni CHADEMA,Chama maarufu kwa maandamano
Afrika Mashariki na kati ni CHADEMA,Uvunjifu wa amani na matukio ya
kigaidi yanatokea kwneye mkitano ya CHADEMA
Na hayo yote ni yale yale waliyokuwa wanayafanya RED BRIGADE wa Italia kuhakikisha serikali na chi haitawaliki.
Slogan ya MOVEMENT for Change na Peoples Power ni mwavuli tu ambao
ulichukuliwa toka Magharibi kuwa ni wanademokrasia,Ili hali ni
wanademogasia
Kwahiyo niseme wazi,mpango huu wanaotaka kuufanya
chadema wa kuunda RB kubwa zaidi tena isiyohitaji msaada wa jeshi la
polisi na Jeshi la Wa Tanzania, ni uhaini, ni ugaidi,ni maandalizi ya
kupindua nchi au kuvuruga kabisa kabisa amani tuliyonayo. Kama
wanavuruga amani na hii Redbrigade ndogo,itakuwaje wakiwa na jeshi.
Naunga mkono kauli ya Rais Mh.Jakaya kikwete hakuna kuundwa kwa jeshi
hilo,na serikali itachukua hatua stahiki kuhakikisha nchi inafuata
misingi ya katiba yake.
Hivyo basi,nawaomba watanzania tuamke,
tusome nyakati kuhusiana na upinzani huu wa CHADEMA wenye mwavuli wa
kisiasa kumbe ni kundi la RedBrigade wa Italy ni hatari kwa nchi yetu.
MWIGULU NCHEMBA,(Mbunge)
0 Maoni/comments: