HII NDO SIMU ITAKAYOKUWA NA 4GB RAM, NA MEMORY YA 128 GB. (UBUNTU EDGE)
Posted in Ubuntu EdgeJanuari mwaka huu Canonical waliitangaza Ubuntu Phone OS kama operating system mpya kwa ajili ya simu, na sasa wanakuletea Ubuntu Edge.
Ubuntu Phone OS ni operating system ambayo inamuwezesha mtumiaji kupata experience ya Ubuntu kwenye simu yake kama ilivyo Windows Phone OS iliyopo kwenye Nokia Lumia.
Canonical, kampuni inayohusika na utengenezaji wa Ubuntu wameenda mbali zaidi kiteknolojia kwa kutangaza Ubuntu Edge, ambayo itakuwa simu ya kwanza kuweza dual-boot operating system mbili kwa pamoja ambazo ni Android na Ubuntu Phone OS.
Android tayari ianjulikana, Ubuntu Phone OS ni operating system ambayo inampa mtumiaji uwezo wa kutumia simu yake kama Kompyuta halisi. Hii itawezekana pale ambapo mtumiaji ata connect simu yake na external screen kama TV kupitia HDMI na atapata Ubuntu Desktop, kwa upande mwingine mtumiaji atatumia Ubuntu Mobile kwa matumizi yake ya kawaida ya simu au Android.
Features
Kutokana na kuwa na uwezo wa kutumika kama kompyuta Ubuntu Edge inatarajiwa kuwa na features zifuatazo.
- kioo chenye inchi 4.5 urefu hanamu 1,280 x 720 HD
- si chini ya 4GB RAM
- 128GB memory
- processor yenye uwezo mkubwa zaidi kuliko zote kipindi itakapotengenezwa (sanasana 8 core)
- kioo cha sapphire crystal (utahitaji kitu kigumu kama almasi kuweka michubuko)
- dual-LTE chip dual-band 802.11n Wi-Fi, Bluetooth 4, NFC
- Betri ya silicon-anode Li- Ion
- dual-band 802.11n Wi-Fi, Bluetooth 4, NFC
- 8mp low-light kamera, 2mp kamera ya mbele
- GPS, accelerometer, gyro, proximity sensor, compass, barometer
- micro sim
- body frame ya chuma
- Upatikanaji
Ubuntu Edge ni toleo maalum kwa watu ambao wangependa kuwa nayo au wapenzi wa teknolojia, hivyo itapatikana kwa wachangiaji wa kampeni ya Ubuntu Edge kupitia Indiegogo.
Source: Bongo Electronics
0 Maoni/comments: