Thursday, May 9, 2013

0

RASMI | DAVID MOYES NDIYE ANAYERITHI MIKOBA YA ALEX FERGUSON | FAHAMU MENGI KUHUSU YEYE KWA KUSOMA HAPA

Posted in , , , , ,

>>SIR ALEX FERGUSON NDIE ALIMPENDEKEZA!!
>>DAVID MOYES: “NI HESHIMA KUBWA! NIMEFURAHI SIR ALEX KUNIPENDEKEZA!”
BODI ya Klabu ya Manchester United imepitisha kwa kauli moja mapendekezo ya Sir Alex Ferguson kuwa David Moyes awe Meneja mpya wa Klabu hiyo na imempa Mkataba wa Miaka 6 utakaoanza Julai 1.
Uteuzi huu unafuatia kutangaza kustaafu kwa Sir Alex Ferguson hapo jana baada ya kukaa Miaka 27 tangu Novemba 1986 lakini atabakia Klabuni hapo kama Mkurugenzi na Balozi.
Akimtangaza Mrithi wake, Sir Alex Ferguson amesema: “Tulipojadili Wagombea wa nafasi ya Umeneja sote tulikubaliana David Moyes anazo sifa zote. David ni Mtu mwenye heshima na mchapa kazi. Nimekuwa nikiihusudu kazi yake kwa muda mrefu na tangu Mwaka 1998 niliwahi kumtaka aje kuwa Meneja Msaidizi hapa. Alikuwa Kijana wakati ule na aliendelea na kazi yake njema huko Everton. Hamna ubishi anavyo vigezo vyote vya kuwa Meneja wa Klabu hii.”
Sir Bobby Charlton alisema: “Siku zote nimesema tunataka Meneja anaefuatia awe Mtu wa Man United wa kweli. Kwa David Moyes tuna Mtu anaeelewa vitu tunavyotaka kuifanya Klabu hii spesheli. Tumempata Mtu ambae atakaa kwa muda mrefu na kujenga Timu za baadae. Uimara hujenga mafanikio.”
David Moyes amesema: “Ni heshima kubwa kuteuliwa kuwa Meneja anaefuatia wa Manchester United. Nimefurahi sana kwamba Sir Alex ndie alienipendekeza kwa kuniona nafaa kwa kazi hii. Ninaheshimu sana vitu vyote alivyofanya na kwa Klabu hii. Najua ni ngumu mno kufuata nyayo za Meneja Bora katika Historia lakini hii nafasi ya kuiongoza Manchester United si kitu kinachokuja kila mara na nangojea kwa hamu kuanza kazi hii.”
David Moyes atatambulishwa rasmi kuwa Meneja wa Man United hapo baadae kwani bado rasmi ni Meneja wa Everton na Mkataba wake unamalizika Tarehe 30 Juni.



DONDOO MUHIMU ZA DAVID MOYES:
Staili ya Timu zake
Siku zote Timu za David Moyes hucheza Soka la Kitimu kwa kushirikiana pamoja na kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika uchezaji wao unaozingatia mbinu, mfumo na kila Mchezaji kumsaidia mwenzake Uwanjani.
Akiwa Everton hakumudu kutwaa Taji lolote  mbali ya kuifikisha Fainali ya FA CUP na kuweza kumaliza 4 Bora na kuwahi kucheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
FERGIE_n_MOYESLakini kila Mwaka, Everton Klabu ambayo haina Fedha, imemudu kumaliza ikiwa katika Timu za juu katika Msimamo wa BPL, Barclays Premier League.
Kimfumo, Moyes hupenda kutumia Staili ya kutumia Straika mmoja tu na Kiungo mmoja akicheza nyuma ya Straika huyo huku Mafulbeki wake wakipanda juu kuongeza nguvu mashambulizi.

DAVID MOYES-==WASIFU WAKE:
JINA KAMILI: David William Moyes
KUZALIWA: 25 Aprili 1963 (Miaka 50)
MAHALI ALIKOZALIWA: Bearsden, Glasgow, Scotland
SOKA POZISHENI ALIOCHEZA: Sentahafu
KLABU: Everton-Ni Meneja

UCHEZAJI:
1978  ÍBV Vestmannaeyjar
1978–1980   Drumchapel Amateurs
1980–1983   Celtic  Mechi 24 Magoli 0   (0)
1983–1985   Cambridge United Mechi 79 Magoli 1
1985–1987   Bristol City Mechi 83 Magoli 6
1987–1990   Shrewsbury Town Mechi 96 Magoli 11
1990–1993   Dunfermline Athletic          Mechi 105 Magoli 13
1993  Hamilton Academical Mechi 5 Magoli 0
1993–1999   Preston North End Mechi 143 Magoli 15
Jumla: Mechi 535 Magoli 46

MENEJA:
1998–2002   Preston North End
2002–2013   Everton
2013– Manchester United F.C.

UMENEJA:
Preston North End
Moyes alianza kazi ya Umeneja Preston North End Januari 1998 Klabu ikiwa taabani Divisheni ya Pili na ikiwa hatarini kuporomoshwa Daraja.
Lakini Moyes, ambae alianza kuchukua Mafunzo ya Ukocha na kupata Beji zake tangu akiwa na Miaka 22 wakati akiwa Mchezaji, aliinusuru Preston kushushwa Daraja na Msimu uliofuata aliiwezeshe kutinga Mechi za Mchujo za kupandishwa Daraja lakini hawakufanikiwa.
Msimu uliofuata Moyes aliifanikisha Preston North End kutwaa Ubingwa wa Divisheni ya Pili na kupanda Daraja kuingia Divisheni ya Kwanza ambako Mwaka 2001 aliifikisha Mechi za Mchujo za kupandishwa Daraja lakini hawakufanikiwa.
Moyes alihama Preston na kwenda Everton Mwezi Machi 2002.
Akiwa na Preston North End, Moyes alisimamia Mechi 243 na Kushinda 113, Kufungwa 63 na Sare 67.
Everton
Moyes alijiunga na Everton hapo Tarehe 14 Machi 200 na Siku aliyotambulishwa rasmi alitamka Everton ni Klabu ya Watu.
Alisema: “Natoka Mji wa Glasgow ambao hauko tofauti na Liverpool. Najiunga na Klabu ya Watu. Watu wengi unaokutana nao mitaani ni Mashabiki wa Everton. Hii ni nafasi safi ambayo Siku zote uniota!”
Mechi yake ya kwanza na Everton ilikuwa ni Goodison Park walipocheza na Fulham na kushinda Bao 2-1.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ