WENGER: CARRICK ANAWEZA KUCHEZA HATA BARCELONA - ANASTAHILI KUWA MCHEZAJI BORA WA ENGLAND MSIMU HUU
Posted in Arsene Wenger, Michael Carrick
ARSENE WENGER amezungumza kwa mara ya kuhusu tuzo ya mchezaji bora wa England msimu huu, akiwashangaza wengi Wenger amemtaja kiungo wa Manchester United Micheal Carrick kuwa ndio mchezaji anayestahili tuzo hiyo msimu huu.
Meneja huyo wa Gunners alisema: “Mimi ningemchagua Carrick. Angeweza hata kucheza ndani ya kikosi cha Barcelonakwa sababu anafiti katika staili ya uchezaji wao.
“Ana uono mzuri na ni mchezaji mwenye akili sana uwanjani."
Mshambuliaji Van Persie mwenye mabao 24 ya Premier League katika mechi 31 alizoanza yamechangia kwa kiasi kikubwa United kuurudisha ubingwa Old Traford - na sasa mdachi huyo anapewa nafasi kubwa ya kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa England.
Lakini Wenger anasema ni mchezaji mwenzie RVP - Carrick, 31, ambaye anastahili kuchukua tuzo hiyo ya PFA.
Aliongeza: “Robin alikaa muda mrefu kidogo bila kufunga. Kura zilipigwa wakati ule hivyo hilo linaweza likaenda dhidi yake.
“Suarez amejiangusha mwenyewe, pia yupo Gareth Bale lakini nadhani hapewi heshima ya kutosha hapa England.
“Muda mwingine sio lazima mfungaji bora awe anazawadiwa - kuna watu nyuma pia. Carrick anastahili. Ningemchagua Carrick kama ilivyokuwa Robin mwaka uliopita. Tuzo apewe mtu mwingine, Carrick ni mtoa pasi bora."
0 Maoni/comments: