SIKU CHACHE BAADA YA KUIBIWA, CHEGE ARUDISHIWA VIFAA VYA GARI LAKE
Posted in Chegge
Baada ya msanii wa kizazi kipya Chege Chigunda kupatwa na msala wa kuibiwa vifaa vya gari lake vinavyo gharimu zaidi ya shilingi milioni 2 hivi karibuni hatimae waliofanya tukio hilo wamerudisha vifaa hivyo kwa hiari.
Akionge na BK Cop Chege amesema watu hao asio wafahamu waliwasiliana nae na kumwelekeza mahala pa’ kuvipatia vifaa hivyo ambapo star huyo alifata maelekezo na hatima kuvipata vifaa vyote vikiwa salama.
Aidha Chege amefafanua kuwa haelewi kwanini watu hao waliamua kufanya tukio hilo na baadae kuamua kurudisha vifaa vyake na kwamba alishafuata taratibu za kisheria hivyo iwapo atabaini alie husika atamfikisha kwenye vyombo vya sheria.
0 Maoni/comments: