FLASH BACK SESSION: UNAWAKUMBUKA NAUGHTY BY NATURE?? (AMERICAN HIP HOP)
Posted in Flashback Session, Naughty By NatureNaughty by Nature ni kundi mshindi wa Grammy Award-wakiwa kama kundi bora la muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Kundi lilitamba sana wakati wa kuanzishwa kwake kunako mwaka wa 1989. Kundi linaunganishwa na msanii kama vile Treach, Vin Rock, na DJ Kay Gee. Kundi lilianzishwa mjini East Orange, New Jersey (kimazungumzo hutajwa kama "Illtown" kunako miaka ya 1980). Kundi lilianza kuonekana kawa mara ya kwanza kwenye uwanja wa muziki mnamo 1989 kwa kutoa albamu yao iliyoitwa Independent Leaders wakiwa chini ya jina lao la awali la New Style. Albamu ikalizalisha kibao ambacho kimepata sifa chache cha "Scuffin' Those Knees". Baada ya kutoa albamu yao ya kwanza, kundi likashauriwa na mzaliwa mwenzao wa huko mjini New Jersey - Queen Latifah, na baadaye wakabadilisha jina lao na kuwa Naughty by Nature.
DJ Kay Gee, Vin Rock na Treach |
Kibao chao cha kwanza Naughty by Nature kuwa maarufu ni wimbo ulioitwa "O.P.P.," ambacho kilichukua samapuli ya kibao cha Jackson 5, "ABC", na kilitolewa mnamo mwaka wa 1991 kutoka katika albamu yao yenye-jina-sawa na lao, Naughty by Nature. Wimbo ulifikia nafasi ya #6 kwenye chati za Billboard Hot 100 [3], ina-kifanya kuwa moja kati ya vibao vilivyopata mafanikio katika historia ya nyimbo za rap kufikia kiwango hicho. Wimbo umepata kujuliakana sana katika tamaduni mashuhuri, kwa kutajwa kwenye vipindi vya TV na filamu kama vile The Fresh Prince of Bel-Air, Malibu's Most Wanted, Monk, na The Office. "O.P.P." pia imepata sifa za juu mno, kwa kutajwa kuwa moja kati ya single bora 100 za rap za muda wote mnamo 1998 na jarida la The Source, and being ranked the 20th best single of the 90s by Spin magazine
Albamu imezalisha kibao kingine kikali cha "Everything's Gonna be All Right" (kibao hiki pia kiliitwa "Ghetto Bastard" katika baadhi ya matoleo kamilifu). Wimbo huo umeelezea maendeleo ya Treach kukulia katika umaskini, na sasa anaishi katika maisha yaliyobora. Nguvu ya mafanikio ya kibao hicho na cha "O.P.P.", imepekea kusukuma albamu kwenda katika platinamu.
Kwa kufuatia mzaliwa mwenzi wao wa New Jersey, Tony D, kuwashataki Naughty by Nature kwa kuiba sampuli ya biti ya albamu yake ya Music Makes You Move na kuitumia kwenye kibao chao cha "O.P.P." Mpango mzima ulikuja kuwekwa sawa mahakamani. Baina ya maalbamu, kundi pia limepata ushindi kabambe na kibao chao cha "Uptown Anthem", kutoka katika kibwagizo cha filamu ya mwaka wa 1992 ya Juice. Treach pia amepata kuuza sura kwenye filamu hiyo, ndiyo mara yake ya kwanza kucheza filamu. Rapa mwenzao 2Pac pia amepata kucheza kwenye filamu hiyo, na Treach akawa rafiki yake. Hii ilimwongoza zaidi kutaka kucheza filamu kwa Treach na urafiki mkubwa na 2Pac. Pale 2Pac alipokufa mnamo mwaka wa 1996, Treach ametengeneza wimbo wa kumuenzi 2Pac, ulioitwa "Mourn You Till I Join You".
Baadaye, kundi likawa na vibao kedekede kutoka katika albamu yao ya tatu ilioitwa 19 Naughty III na Poverty's Paradise pekee. Albamu zote mbili zimefikia #1 kwenye chati za R&B/Hip-Hop Charts. "Hip Hop Hooray" ulikuwa wimbo wenye mafanikio kutoka katika albamu ya 19 Naughty III. Video yake iliongozwa na Spike Lee na imehusisha wasanii wengine maarufu wa hip hop wa mwanzoni mwa miaka ya 1990, ikiwa ni pamoja na Queen Latifah, Eazy-E, Run-D.M.C., na Da Youngstas. Poverty's Paradise imeshinda tuzo ya Grammy Award mnamo mwaka wa 1996 ikiwa kama Albamu Bora ya Rap, na kibao kikali kutoka humo kilikuwa "Feel Me Flow" ambacho kimeshika nafasi ya #17 kwenye chati za Billboard Hot 100.
SOURCE: WIKIPEDIA.
0 Maoni/comments: