CORINTHIANS VS CHELSEA: FIFA CLUB WORLD CUP FINALS-TATHMINI
Posted in Chelsea, Corinthians, Fifa Club World Cup
>>JUMAPILI Desemba 16, Saa 7 na Nusu Mchana
>>UWANJA: NISSAN, YOKOHAMA, JAPAN
NI
FAINALI ya Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani na
yanazikutanisha Klabu ya Brazil, Sport Club Corinthians Paulista, ambao
ni Mabingwa wa Marekani ya Kusini baada ya kutwaa Copa Libertadores,
dhidi ya Klabu ya England, Chelsea, ambao ni Mabingwa wa Ulaya, baada ya
kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mashindano haya, Timu zote hizi
mbili zilianzia hatua ya Nusu Fainali na Corinthians waliwatoa Al Ahly
kwa Bao 1-0 na Chelsea kuifunga Monterrey Bao 3-1.
Kabla ya Mechi ya Fainali kuanza, hapo
Saa na Nusu Asubuhi, Mabingwa wa Afrika, Al Ahly, watachuana na
Monterrey ya Mexico katika Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu wa Mashindano
haya.
+++++++++++++++++++++++
VIKOSI VINATARAJIWA:
Sport Club Corinthians Paulista [Mfumo: 4-2-2-2]:
Cassio
Alessandro, Chicao, P Andre, F Santos
Paulinho, Ralf
Danilo, Douglas,
Guerrero, Emerson
Chelsea [Mfumo:4-2-3-1]:
Cech
Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole
Mikel, Luiz
Mata, Oscar, Hazard
Torres
+++++++++++++++++++++++
Kila Timu itaingia kwenye Mechi hii bila
majeruhi ingawa Chelsea inao majeruhi wa muda mrefu, Daniel Sturridge
(Musuli ya Pajani), John Terry (Goti) na Oriol Romeu (Goti), na ambao
hawapo huko Japan.
Kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali,
huenda Beki David Luiz akachezeshwa kwenye Kiungo ambako alicheza vizuri
dhidi ya Monterrey.
Kocha
Corinthians Tite anategemewa kuendeleza Mfumo wake wa 4-2-2-2 ambao
ulimpa mafanikio makubwa kwenye Mashindano ya Copa Libertadores ili umpe
Taji lao la Pili la Klabu Bingwa Duniani baada ya kutwaa Taji la kwanza
katika Mashindano ya kwanza kabisa Mwaka 2000.
+++++++++++++++++++++
MABINGWA WALIOPITA:
-2000 - Corinthians
-2005 - Sao Paulo
-2006 - Internacional
-2007 - AC Milan
-2008 - Manchester United
-2009 - Barcelona
-2010 - Inter Milan
-2011 – Barcelona
++++++++++++++++++
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA/MATOKEO:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
Sanfrecce Hiroshima 1 Auckland City 0
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
Usain Hyundai 1 Monterrey 3
Sanfrecce Hiroshima 1 Al Ahly 2
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai 2 Sanfrecce Hiroshima 3
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly 0 Corinthians 1
Desemba 13, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey 1 Chelsea 3
MSHINDI wa 3
Desemba 16
[Uwanja wa Yokohama]
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Al Ahly v Monterrey
FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Corinthians v Chelsea
0 Maoni/comments: