CECAFA CHALLENGE CUP 2012 (KILI STARS YANYUKWA-BURUNDI YATINGA ROBO FAINALI) Kutoka SOKA-IN-BONGO
Posted in CECAFA TUSKER CUP, Kilimanjaro Stars
>>ALHAMISI: Zanzibar v Rwanda!!
LEO, kweye michuano ya kusaka Nchi
Bingwa ya Afrika Mashariki na ya Kati, CECAFA TUSKER CHALENJI CUP 2012
huko nchini Uganda, katika Mechi ya Kundi B, Kilimanjaro Stars,
imechapwa Bao 1-0 na Burundi, kwa Bao la Penati, na kuifanya Burundi iwe
Timu ya pili kutinga Robo Fainali baada ya jana Wenyeji na Mabingwa
watetezi, Uganda, kufanya hivyo pia.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A: Uganda, Ethiopia, Kenya, South Sudan
KUNDI B: Sudan, Tanzania, Burundi, Somalia
KUNDI C: Rwanda, Malawi, Zanzibar, Eritrea
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Penati iliyowaua Kilimanjaro Stars
ilisababishwa na Shomari Kapombe na kufungwa kifundi na Ndikumana
Suleiman katika Kipindi cha Pili.
Katika Mechi nyingine ya Kundi B ambayo pia ilichezwa leo, Sudan iliichapa Somalia Bao 1-0.
Michuano hii itaendelea Alhamisi Novemba
29 kwa Mechi za pili za Kundi C kwa Zanzibar kucheza na Rwanda, na
Eritrea kucheza na Malawi.
RATIBA/MATOKEO:
KUNDI A:
Novemba 24: Ethiopia 1 South Sudan 0, Uganda 1 Kenya 0
Novemba 27: South Sudan 0 Kenya 2, Uganda 1 Ethiopia 0
Novemba 30: Kenya v Ethiopia, South Sudan v Uganda
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Uganda Pointi 6
2 Kenya 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Ethiopia 3 [Tofauti ya Magoli: 0]
4 South Sudan 0
KUNDI B:
Novemba 25: Burundi 5 Somalia 1, Tanzania 2 Sudan 0
Novemba 28: Somalia 0 Sudan 1, Tanzania 0 Burundi 1
Desemba 1: Sudan v Burundi, Somalia v Tanzania
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Burundi Pointi 6
2 Kili Stars 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Sudan 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
4 Somalia 0
KUNDI C:
Novemba 26: Zanzibar 0 Eritrea 0, Rwanda 2 Malawi 0
Novemba 29: Malawi v Eritrea, Rwanda v Zanzibar
Desemba 1: Malawi v Zanzibar, Eritrea v Rwanda
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 1]
1 Rwanda Pointi 2
2 Zanzibar 1
3 Eritrea 1
4 Malawi 0
FAHAMU: Washindi wawili wa juu wa kila Kundi pamoja na Timu mbili zitakazoshika nafasi za 3 Bora zitaingia Robo Fainali.
ROBO FAINALI: Desemba 3 & 4
NUSU FAINALI: Desemba 6
FAINALI: Desemba 8
0 Maoni/comments: