Saturday, September 8, 2012

0

“REDIO NA TELEVISHENI ZINAUSAHAU MUZIKI WA DANCE” – ALLY CHOKI…!!

Posted in ,
Extra Bongo Kazini
MKURUNGEZI wa bendi ya muziki wa dance ya Extra Bongo ‘Next Level’, Ally Choki, amesema kuwa vyombo vingi vya habari hasa Redio na Televisheni zinausahau muziki wa dance tofauti na miaka ya zamani nyakati ambazo muziki huo ulikuwa na nguvu.

Choki alifanya mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye alitaka kujua muziki huo kwa sasa upo kwenye kiwango gani tofauti na miaka ya nyuma, ambapo alidai kuwa muziki unasonga mbele lakini kwa upande fulani vyombo hivyo vya habari vinausahau.




Alisema kuwa hasemi kwamba wapige muziki nyimbo za muziki wa dance muda wote hapana lakini bado mpangilio wa vipindi vya muziki huo hauna nguvu kama ulivyo wa muziki wa bongo fleva ambao hupowa na nafasi kubwa.

“Miaka ya nyuma muziki wa dance ulikuwa na nguvu kubwa sana si kama sasa na hii naweza kusema baadhi ya vyombo vya habari kama redio na televisheni zina sahau kuupa nafasi,” alisema.

Choki alitoa maoni yake kwa wadau wote wa muziki nchi kuupa nafasi muziki wa dance.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ