Aug
2012
13
Tanzania Isiyo Na Medali Za Olympic
Posted in London Olympics 2012
1.Kwenye SWIMMING,yale maji yao yalikuwa ya moto kweli,kushinda hata ya Coco beach tulipofanyia mazoezi,maji utasema uko bafuni unaoga halafu marumaru zile zinapendeza hadi zinachanganya
2.Kwenye MARATHON,barabara zao zina mikunjo mingi sana kama za Kampala na Nairobi ndo maana Kenya na Uganda walishinda..sisi tumezoea za one way kama Mwenge-Posta
3.Kwenye BOXING,wale watu wao wana sura za kitoto na warembo sana hadi unaogopa kuwapiga unaweza kupata kesi
Yasingekua hayo mambo tuliyoyataja tungerudi na Gold kwenye michezo yote!Ikitokea ya nchi nyingine msisite kutuita tukajaribu tena!!
0 Maoni/comments: