Jul
2012
05
Steve Nyerere amkabidhi Mama Maria Nyerere Zawadi ya Movie
Posted in Bongo Movies, Steve NyerereSteve alisema kwamba kumpa filamu hiyo ni kuweka kumbukumbu kwamba, anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi.
Amesema, Mama Maria Nyerere alimsaidia sana kujifunza mengi kumhusu baba wetu wa taifa ikiwemo kumuonyesha vitu gani Mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani mwalimu alikuwa akivipenda,na hata na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake.
Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambao walijitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo ilikamilika.
- Mama Maria Nyerere akisalimiana na msanii Steve Nyerere
- Mama Maria Nyerere akionyesha filamu aliokabidhiwa kama zawadi
- Wsanii na mama Maria Nyerere kwenye picha ya pamoja
- Mama Maria Nyerere akizungumza
- source: bongo5.com
0 Maoni/comments: