Next
Previous
Showing posts with label Azam FC. Show all posts

Wednesday, November 27, 2013

0

JICHO ANG'AVU JUU YA AZAM TV | ANGALIZO

Posted in ,

AzamTV is a digital satellite service provider, top quality family entertainment at a single affordable
$R7BA1SX
Jengo La Azam Tv
price. The headquarters are located in Dar-es-Salaam, Tanzania where it was founded in 2013 with
the intention to expand across other countries in Africa in the near future.
Our vision is to offer a wide range of programmers consisting of both international and local channels
suitable for families, sports fans and individuals of all ages across Tanzania.
Viewers can also record programmers while watching them with on to a USB device. Naturally the
decoder comes with an HDMI connection option for that perfect picture on your TV.

Why choose Azam TV?
• Azam TV is a household name renowned for offering great service to the Tanzanian people at
an affordable price.
• Our commitment is to offer the best quality service and entertainment in your home on a pay
as you go basis.
• We love what we do, our digital television service is quick and easy to install and use
• If you are looking for a digital service to trust, Azam TV is what you need, it’s so easy to switch!

Azam One – Local Entertainment Channel description?
Watch all your favourite award-winning dramas, African movies, the Tanzanian Premier League
football matches and kids entertainment in the comfort of your own home once you get Azam TV
installed.

Thursday, August 15, 2013

0

NI YANGA VS AZAM WEEKEND HII | NGAO YA JAMII - MATCH REPORT

Posted in ,

Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga na makamu bingwa Azam wanavaana keshokutwa (Jumamosi) kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu 2013/2014.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa ngao.

Iwapo dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.

Sunday, May 5, 2013

0

MCHEZAJI BORA WA MWAKA TANZANIA: AZAM YATAWALA

Posted in


AZAM FC imeingiza wachezaji wawili katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora kwenye Tuzo za Wanamichezo Bora Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) 2012/2013 ambao ni Khamis Mcha ‘Vialli’ na John Bocco ‘Adebayor’.
Katika kipengele hicho, nyota hao wawili wa Azam watachuana na Kevin Yonda wa Yanga, Shomary Kapombe wa Simba anayeshikilia tuzo hiyo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, wote wa TP Mazembe ya DRC.
Azam imeingia mchezaji mmoja katika kipengele cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kigeni anayecheza Tanzania, ambaye ni Kipere Herman Tchetche kutoka Ivory Coast atakayechuana na Mganda Emmanuel Okwi aliyekuwa Simba kwa sasa ameuzwa Etoile du Sahel ya Tunisia.
Katika kipengele hiki, Yanga SC imeingiza wachezaji wawili ambao ni Haruna Niyonzima kutoka Rwanda na Hamisi Kiiza kutoka Uganda.
Upande wa wanasoka wa kike, Fatuma Mustafa atachuana na Asha Rashid, Mwanahamisi Omary, Sofia Mwasikili anayeshikilia tuzo huyo na Esther Chabruma.
Katika mpira wa magongo wanaume Sylvester Kigodi atachuana na Castor Mayuma, Gurtej Bilu Singh, Vendri Bhamra na Elias Samala. Gofu ya Kulipwa; Hassani Kadio, Yassin Salehe, Fadhili Nkya, Salimu Mwanyenza na Rajabu Iddy.

Sunday, April 21, 2013

0

NA SOKA IN BONGO: VPL-YANGA 3 JKT RUVU 0, YANGA BADO POINTI 1 BINGWA!!

Posted in , ,
>>YANGA BADO COASTAL, SIMBA!!
>>LAKINI, AZAM AKIFUNGWA NA COASTAL JUMAMOSI IJAYO, YANGA BINGWA!!
Vinara wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga leo wameipiga JKT Ruvi Bao 3-0 na kujiweka nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa kwa kuhitaji Pointi 1 tu kati ya Mechi 2 walizobakisha bila ya kujali matokeo yeyote ya Timu ya Pili Azam FC.
+++++++++++
MAGOLI:
Yanga 3
-Simon Msuva Dakika ya 45
-Hamis Kiiza 59
-Nizar Khalfan 65
JIK Ruvu 0
+++++++++++
Yanga sasa imefikisha pointi 56 wakifuatiwa na Azam FC wenye Pointi 47 na waliobakisha Mechi 3.
++++++++++++++++++++++++++++
MECHI WALIZOBAKISHA YANGA:
Mei 1: COASTAL v YANGA YANGA [MKWAKWANI]
Mei 18: YANGA v SIMBA [UWANJA wa TAIFA]

Tuesday, February 12, 2013

0

PICHA AZAM WAKIFANYA MAANDALIZI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

Posted in ,

Saturday, October 27, 2012

0

YALIYOJIRI LIGI KUU TANZANIA BARA NA RATIBA YA MECHI ZIJAZO:: NA WENZETU SOKA IN BONGO

Posted in , , , ,

VPL: Simba yaipiga Azam, Yanga yaipiku Azam nafasi ya 2!!

Jumamosi, 27 Oktoba 2012 20:14
Chapisha Toleo la kuchapisha
VPL_LOGOKatika mfululizo wa Mechi za Ligi Kuu Vodacom, VPL, zilizochezwa leo, Mabingwa watetezi Simba wamefanikiwa kuichapa Azam bao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuendelea kubaki kwenye uongozi huku Yanga, wakiwa huko Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakiifunga JKT Oljoro bao 1-0 na kuipokonya Azam nafasi ya Pili kwenye Msimamo wa Ligi.
++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO/RATIBA:
Oktoba 27
Simba 3 Azam 1
JKT Oljoro 0 Yanga 1
African Lyon v Kagera Sugar
Mgambo JKT v Tanzania Prisons
Ruvu Shootings v Polisi Morogoro
++++++++++++++++++++++++++
Bao la ushindi la Yanga lilifungwa na Mbuyu Twite katika Dakika ya 53.
Katika Mechi ya Simba na Azam, John Bocco ndie alietangulia kuifungia Azam bao moja katika Dakika ya 5 lakini Simba ikazinduka na kupiga Bao 3 kupitia Felix Sunzu, Dakika ya 7, na bao mbili za Emmanuel Okwi.
++++++++++++++++++++++++++

Saturday, October 6, 2012

0

MPYA ZA LEO KUTOKA TFF, Na Wenzetu SOKA-IN-BONGO

Posted in , , , , , ,
>> YANGA, AFRICAN LYON KUTOVAA BEJI YA MDHAMINI!
>> WAAMUZI WATATU WAONDOLEWA, SIMBA YAPIGWA FAINI!
>> MECHI YA KAGERA SUGAR, YANGA YASOGEZWA!
>> LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 20!

LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 20
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Oktoba 5 mwaka huu) kupitia na kufanya uamuzi katika masuala mbalimbali na kupanga Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ianze kutimua vumbi Oktoba 20 mwaka huu.
TFF_LOGO12Timu zimepangwa katika makundi matatu ya timu nane nane ambapo zitacheza ligi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Mshindi wa kila kundi ndiye atakayepata tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao wakati timu ya mwisho kila kundi itashuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa.
Kundi A lina timu za Burkina Moro ya Morogoro, Kurugenzi Mufindi ya Iringa, Majimaji ya Songea, Mbeya City ya Mbeya, Mlale JKT ya Ruvuma, Mkamba Rangers ya Morogoro, Polisi Iringa na Small Kids ya Rukwa.
Ndanda FC ya Mtwara, Ashanti United, Green Warriors, Moro United, Polisi, Tessema, Transit Camp na Villa Squad zote za Dar es Salaam ndizo zinazounda kundi B wakati kundi C ni Kanembwa JKT ya Kigoma, Morani ya Manyara, Mwadui ya Shinyanga, Pamba ya Mwanza Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers ya Tabora.
Ada ya ushiriki wa ligi ni sh. 200,000 zinazotakiwa kulipwa kabla ya Oktoba 13 mwaka huu. Pia Oktoba 13 mwaka huu kutakuwa na kikao kati ya wenyeviti wa klabu zote zinazoshiriki ligi hiyo na Kamati ya Ligi ambapo pia itafanyika draw (ratiba).

Wednesday, August 1, 2012

0

Mrisho Ngassa Asababisha Kocha wa Azam kutimuliwa

Posted in , , , ,

STEWART Hall, kocha Muingereza wa Azam FC jana amefukuzwa rasmi katika klabu hiyo kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame. Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Azam, zimesema kwamba kikao cha jana cha pamoja baina ya Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC, Mwanasheria wa kampuni na kocha
Stewart kimeafiki kuvunj ndoa hiyo na sasa Azam FC itakuwa chini ya kocha
kutoka India, Vivek Nagul ambaye alikuwa anafundisha timu ya vijana.
Habari zinasema kwamba mapema baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kagame, kati ya Azam na AS Vita ya DRC, Stewart aliitwa na kuambiwa asimtumie tena Ngassa kwa kitendo cha mchezaji huyo kwenda kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga, baada ya kufunga bao la ushindi.
Lakini Stewart katika kikao hicho, kwanza alimtetea Ngassa kutokana na
kufunga bao la ushindi na\ kumuelezea kama mchezaji
muhimu kwake, lakini msimamo wa bodi ulikuwa
ni asipangwe tena. Katika fainali, Stewart
alimvalisha jezi Ngassa akamuanzishia benchi, lakini
kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali alimuingiza
kipindi cha pili timu ikiwa nyuma kwa 1-0 na mwisho
wa mchezo ikashinda 2-2 yeye akifunga la pili, dhidi
ya Yanga pia alimuingiza timu ikiwa nyuma kwa 1-0.
Lakini Ngassa alishindwakurudia kile alichofanya kwenye mechi na AS Vita na
Yanga ikashinda 2-0. Kwa sasa mazungumzo
yanaendelea kati ya Yanga na Azam juu ya Ngassa ili
mchezaji huyo arejee Jangwani, lakini wakati huo
huo, Simba nao wameweka dau la Sh. Milioni 25 katika
50 zinazotakiwa na Azam ili kumuuza mchezaji huyo.
Mbali na Ngassa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’
pia yuko katika wakati mgumu na jana inadaiwa
alionekana akilia wakati anazungumza na kiongozi
mmoja wa Azam, akiuliza ni lipi kosa lake.
Sure Boy, ambaye ni mtoto wa kocha wa timu ya vijana
ya Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ jana hajafanya
mazoezi na leo pia, naye pia akituhumiwa kucheza kinazi
katika mechi dhidi ya Yanga. Stewart anakuwa kocha wa
nne ndani ya miaka minne kufukuzwa Azam, tangu
Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin,
Mbrazil mwingine. Lakini ni Stewart angalau
anaacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada
ya kuiwezesha kutwa Kombe la Mapinduzi Januari,
kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya
kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame mwezi
uliopita

Friday, July 27, 2012

0

Nani Kuibuka Kidedea??: Yanga VS Azam

Posted in , , ,
Ijumaa, 27 Julai 2012 11:59
Chapisha Toleo la kuchapisha
  • KAGAME_CUP_2012• NANI kulikwaa ‘BUTI la DHAHABU??’
Jumamosi Julai 28 Fainali ya Kagame Cup, Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa Mechi kati ya Mabingwa watetezi Yanga na Azam FC.
Hakuna Mdau yeyote wa Soka mwenye uhakika kama Yanga watafanikiwa kutetea vyema Taji lao walilolitwaa Mwaka jana kwa kuwafunga Mahasimu wao Simba bao 1-0 kwenye Fainali au Timu mpya kwenye Mashindano haya, Azam, inaweza kujiwekea historia kwa kulibeba Kombe hili kwa mara ya kwanza.
Uhakika pekee uliokuwepo ni kuwa Kagame Cup inabaki tena Tanzania kwa mara ya pili mfululizo.
==========================
WAMEFIKAJE FAINALI:
YANGA
KUNDI C:
-Atletico 0-2
-El Salaam Wau 7-1
-APR 2-0
ROBO FAINALI:
-Mafunzo 1-1 [Penati 5-3]
NUSU FAINALI:
-APR 1-0 [Baada ya Dakika 120]
AZAM
KUNDI B:
-Mafunzo 1-1
-Tusker 0-0
ROBO FAINALI:
-Simba 3-1
NUSU FAINALI:
-Vita Club 2-1
==========================
YANGA-AZAM3NATIONAL_STADIUM2Hakika Fainali hii ni ngumu na imezua mjadala mkubwa hasa ikikumbukwa mara ya mwisho Timu hizi kukutana ilikuwa ni kwenye Ligi Kuu Vodacom Mechi ambayo Azam walishinda bao 3-1 lakini Mechi hii ilizua balaa kubwa baada kutokea vurugu kwa Mwamuzi Israel Nkongo mara baada ya kumpa Kadi Nyekundu Niyonzima wa Yanga na kusababisha Wachezaji kadhaa wa Yanga kupigwa Faini na kufungiwa kwa madai ya kumpiga Refa huyo.
==========================
WAGOMBEA ‘BUTI la DHAHABU’:
-Teddy Etekiama [Vita Club]=Bao 6
-Said Bahanuzi [Yanga]=5
-Hamisi Kiiza [Yanga]=5
-John Bocco [Azam]=5
-Suleiman Ndikumana [APR]=3
-Preus [APR]=2
-Abdallah Juma [Simba]=2
==========================
Mbali ya kuwa na Timu zilizosheheni Wachezaji mahiri Timu hizi pia zina Mastraika hatari mno ambao pia wana vita kubwa kati yao ya kuwania Tuzo ya Mfungaji Bora kwenye michuano hii ambayo hadi sasa alieshika Nambari Wani kwenye safu ya ufungaji ni Teddy Etekiam wa Vita Club mwenye Bao 6 na anafukuzwa na Wachezaji watatu wenye Bao 5 kila mmoja ambao ni Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza wa Yanga na John Bocco wa Azam.
Wachezaji wote hawa wana nafasi nzuri ya kuongeza Mabao wakati Timu zao zitakapocheza Fainali na ile Mechi ya kutafuta Mshindi wa Tatu.
RATIBA:
MSHINDI WA 3:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 8 Mchana]
Vita v APR
FAINALI:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 10 Mchana]
Azam v Yanga
KWA RATIBA na HABARI NYINGINE BOFYA: http://www.sokainbongo.com/kagame-cup-2012
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ