Dec
2013
20
KAMA HUWEZI YA RAMA DEE NA JAY DEE KUFANYIWA VIDEO NDANI YA NCHI TATU
Posted in Lady Jay Dee, Rama DeeMsanii mkongwe wa r&b Bongo, Rama Dee ambaye anamiliki tuzo ya wimbo bora wa RnB aliyoichukua kupitia wimbo wake wa ‘Kuwa na subira’, ambaye kwa sasa maskani yake yapo sana Australi ambapo anaisi na mkewe wakiwa na mtoto mmoja amefunguka juu ya mpango wake wa kushuti video ya ‘Kama huwezi’.

“Nia yangu ipo palepale kwamba ‘Kama Huwezi’ itahusisha nchi tatu kama location ya video hiyo. Nchi hizo ni hapa Australia, South Africa ambapo ndege nitakayopanda kuja nayo Dar itapita na kukaa muda mrefu kabla ya kuja huko na mwisho ni Tanzania jijini Dar es salaam ambapo ndipo hata shot zote za Jide zitapigwa hapo.” – Rama Dee.
“Sasa tatizo ninalokutana nalo ni kwamba kwenye hizi nchi nyingine wanahitaji muda mrefu sana hadi kufanya video kwa uhuru hadi waangalie kwanza video zetu huwa zina nini hasa but lazima nitafanya na pia zipo video nyingi sana ambazo nimeshazifanya zinakuja, kwa kifupi fans wangu wategemee makubwa kutoka kwangu na uzuri kwa sasa nipo likizo ya masomo yangu ya muziki ambayo nimeamua kusomea ili kujiongezea ujuzi zaidi.” – Rama Dee.
0 Maoni/comments: