Nov
2013
27
UKWELI JUU YA ISHU YA SNURA NA MRISHO NGASSA HUU HAPA
Posted in Mrisho Ngassa, Snura
Ni picha ambazo zimekua zikizungumziwa kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye mitandao mingine ya habari nchini Tanzania zikimwonyesha mchezaji wa Yanga Mrisho Ngassa akiwa mapenzini na mwimbaji Snura wa bongofleva.
‘Simu yangu ilipotea ndio maana wamezipata hizo picha, wakati tunashoot tulikua tunapigapiga tu hayo mapicha, mi sikuwa nataka kuzitoa kabisa manake movie yenyewe bado naifanya nusunusu kutokana na kukosa muda, hii ishu imeniletea sana matatizo manake mwingine anakua haamini unachokiongea na hakuna kitu kinauma kama kuongea ukweli alafu mtu anasema unadanganya’ – Snura
Kwa kumalizia Snura anasema ‘Ngassa alinipiga muda mfupi tu baada ya picha kuanza kusambaa akauliza mbona hizi picha zinasambaa hivi Snura? nikamwambia usinielewe tofauti babaangu kwa sababu mimi mwenyewe sikutaka zitoke, picha nilizopiga nyinginyingi tu wakati tunatengeneza movie ila naona watu wameona hizi ndio nzuri kwa skendo’
0 Maoni/comments: