
Kutokana na hali ya Msanii
Sadick Juma Kiwolo au maarufu kama
Sajuki
kuendelea kuwa mbaya serikali imeamua kuingilia kati swala hilo na
kuchukua uamuzi wa kumsaidia kimatibabu msanii huyo hadi pale atakapo
pata nafuu.
Sajuki ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya
Muhimbili na amegundulika kuwa anatatizo la kufeli kwa
Figo na kwamba yuko chini ya uangalizi na uchunguzi zaidi.
Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Wilson Makubi amesema kuwa serikali imejitolea kumsafirisha msanii huyo kwa gharama zote pamoja na gharama za matibabu akiwa nchini
India. Sajuki anatariwa kusafiri wiki ijayo baada ya taratibu zote zitakapo kamilika.
0 Maoni/comments: