RIP MUIGIZAJI MNAIGERIA: MZEE PETE ENEH
Posted in Nollywood, Pete EnehMuigizaji mkongwe wa filamu nchini Nigeria Pete Eneh amefariki dunia.
Eneh amefariki juzi ikiwa ni siku chache baada ya mguu wake mmoja kukatwa kutokana na kuambukizwa ugonjwa katika hospitali Park Lane mjini Enugu.
Afya yake ilidaiwa kuwa mbaya baada ya kukatwa mguu huo.Mguu wake ulianza kuoza baada ya kujeruhiwa mwaka jana amapo hakuweza kupata matibabu stahili na hivyo mguu ulikatwa ili kuzuia maambuziki yasisambae mwili mzima.
Katika maisha yake ya Nollywood, Eneh aliigiza kwenye filamu takriban 98 zikiwemo “Lonely Life”, “Divided Kingdom”, “Prize of Ignorance”, “Heavy Rain”, “Naomi “, “Not Your Wealth,” “Return of Odo,” “Prince,” “Demon in law,” na “Blind couple”.
0 Maoni/comments: