HAWAFUNDISHWI UKAHABA WAKIINGIA BONGO MOVIE-'ASEMA JACK WA CHUZI JUU YA WANAWAKE WANAOJIUNGA BONGO MOVIE'
Posted in Jackline PentzelMSANII wa filamu bongo Jackline Pantzel maarufu ‘Jack wa Chuzi’, amefunguka na kueleza kuwa ndani ya tasnia yao hakuna mwanamke changudoa au muhuni na kama yupo basi huyo alikuwa na tabia hiyo hata kabla hajaingia katika fani hiyo.
Kauli ya msanii huyo inaweza kuwa na ukweli ndani yake kwani wasanii wengi wametoka sehemu mbalimbali ndani ya taifa hili, hivyo inawezekana uchangudoa alikuwa nao kitambo lakini hakuna anayefundishwa tabia hiyo akiingia bongo movie.
Msanii huyo alisema kuwa wasanii wote ni watu wazima na wana akili zao timamu hivyo wanaopenda kuitwa wahuni au changudoa basi hao watakuwa na kasoro kwani wapo baadhi hawafanyi filamu ili kujiuza kama watu wanavyodai na kikubwa ni kuelimisha hasa kwa wale wanaopenda kutazama kazi zao.
“Hakuna msanii wa kike anayefundishwa ukahaba ndani ya bongo movie na kama yupo aliyewahi kufundishwa basi awataje waliomfundisha, nachoelewa mimi ni kwamba kama yupo msanii wa kike changudoa basi tabia hiyo alianza hata kabla hajaigia kufanya filamu,” alisema.
Jack alidai kuwa zipo taarifa kadhaa ambazo zimekuwa zikidai kuwa baadhi ya wasanii wa bongo movie ni machangudoa lakini ishu hizo huwa zinawagusa wote, wakati wahusika wakuu wa tabia hizo ni wale ambao wametoka kwenye mashindano fulani ya urembo.
0 Maoni/comments: