SHILOLE NAYE AKAA UCHI: Hii Tabia Sijui Wabongo Wameitoa Wapi??
Posted in Jokate Mwegelo, Shilole, Wema Sepetu
Mpaka sasa tuna picha zinazomwonesha Shilole ambaye kwa sasa amegeukia muziki wa mduara, akiwa jukwaani huku akionekana hana habari kabisa na kitu kinachoitwa staha achilia mbali heshima.
Chanzo chetu cha habari kwa sharti la kutotajwa jina lake , kilinyetisha kwamba, Shilole amekuwa na kawaida ya kujiachia kihasarahasara hasa anapokuwa kwenye shoo na bendi yake.

Mdau wa filamu Jumanne Athuman, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam, alisema amekerwa sana na kitendo cha Shilole kukaa hovyo jukwaani kwani anajidhalilisha mbele ya jamii ambayo itajitizama kupitia kwake.
“Huyu Shilole hana heshima kabisa, juzi tu nilisoma katika mitandao akiwakashfu Wema na Aunt eti ndiyo tatizo Bongo Movies, mbona naye huwa anajiachia hovyo?
“Kwa nini hawa wasanii hawajiheshimu? Inaniuma sana, nahisi kama ndiyo kawaida yao. Ni sikio la kufa…hawasikii dawa. Wamezidi sana, wanajichafulia heshima zao kwenye jamii,” alisema Jumanne
0 Maoni/comments: