Sunday, August 4, 2013

0

CHUO KIKUU CHALEA MAKAHABA: NI CHUO KIKUU DODOMA AMBACHO KIMEENDELEA TAWALIWA NA HAWA MADADA POA

Posted in ,


Ongezeko  la  makahaba  mjini  Dodoma  limeendelea  kuwa  kero  kwa  chuo  kikuu  cha Dodoma  na  wanafunzi  wake  kwa  ujumla....

Kero  hiyo  imekuwa  ikisababishwa  na  baadhi  ya  makahaba  hao  kujifanya  wanafunzi  wa  chuo  hicho  kwa  lengo la kujiimarisha  kibiashara...

 Takribani miezi mitatu  iliyopita, kahaba mmoja alinasawa  na polisi   mjini Dodoma akijiuza kwa  kujinadi  kuwa  yeye  ni  mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dodoma ..

 Baada  ya  mahojiano  ya  kina  na Polisi Central,  ilibainika  kuwa  kahaba  huyo  hakuwa  Mtanzania  na  hakuwa  mwanafunzi  wa  chuo  chochote  hapa  nchini  na  badala  yake  alikuwa  ni  raia  wa  Malawi.

Upekuzi wa polisi  ulifanikiwa  kunasa  ARVs  za  kupunguza  makali  ya  virusi  vya  UKIMWI  toka  kwa  mwanamke  huyo  aliyekuwa  akiendesha  maisha  yake  kwa  kuuza  mwili  wake  maeneo  ya  Uhindini  mkoani  humo.

 Mbali  na  ushahidi  huo, mtandao huu  umefanikiwa  kumnasa  binti  mwingine  anayejiita  SECHE  MAUTAMU...


Seche  ni  binti  aliyeamua  kujiuza  kupitia  mtandao  wa  facebook  kwa  kuwalaghai  wanaume  kwamba  yeye  ni  mwanafunzi  wa  UDOM....

Hata  katika  profile  yake, binti  huyo  ameweka  wazi  kuwa  yeye  ni  mwanafunzi  wa  UDOM  huku  ukurasa  wake  ukipambwa  na  picha  kadhaa  za  uchi.....

Kinachotia  shaka  ni  kwamba, picha  zote  25  zilizowekwa  hazithibitishi  moja  kwa  moja  kwamba  Seche  ni  mwanafunzi  ama  wa  UDOM au  chuo  chochote  cha  Tanzania...

Picha  zilizowekwa  ni  za  gheto lake akiwa  UCHI, hali  inayotia  shaka  kubwa  ya  kukubaliana   na  uanafunzi  wake  wa  UDOM....

Ili  kuupata  ukweli  wa  mambo, mtandao huu  ulizungumza  na  wanafunzi  10 toka  chuoni  hapo  kwa  nyakati  tofauti..

Miongoni  mwa  wanafunzi  tulioongea  nao  ni  wale  waliomaliza  mwaka  2013, 2012 na 2011.  Wanafunzi  wote  10  wameshindwa  kumtambua  Seche  na  kudai  kuwa  huyo  ni  kahaba  aliyeamua  kuwachafua....

"Huyo siyo  mwanafunzi, ni  kahaba   ambaye  ameamua  kutuchafua. Kama  kweli  ni  mwanafunzi, mwambieni  aweke  japo  picha  moja  tu  akiwa  katika  mazingira  ya  chuo  cha  UDOM"...Alisema  mmoja  wa  wanafunzi  hao.

Kwa  kipindi  cha  mwaka  mmoja, mkoa  wa  Dodoma  umekubwa  na  ongezeko  kubwa  la  MALAYA  wanaoishi  kwa kuuza  miili  yao..

Maeneo  makubwa  yaliyoathiriwa  na  makahaba  hao  ni Chako ni chako, Uhindini,eneo la ofisi za hood karibu na club moja ya usiku na  maeneo ya ukumbi wa 84.

Cha  kushangaza  ni  kwamba  malaya  wote  hujiita  wanafunzi  wa  UDOM.Wakiulizwa  kozi  wanazosoma  huishia  kujiuma  na  kuwa  wakali .

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ